Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 11/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 11/2025

SIKU 17 YA 30

Kutegemea msaada kutoka kwa watu ni kukwepa kulipa gharama ya kumfuata Mungu, ambayo ni kumtazama yeye, kutubu, na kuziacha njia mbaya. Unapokumbana na matatizo ya kimaisha ni vema ukachukua hatua ya kuwasiliana na Mungu ili ushauriwe na kukumbushwa maagizo yake. Uongozi wa Mungu unatufanya tuikatae na kuitupa miungu ambayo si kitu kwa Mungu. Miungu hutuletea matumaini bandia na ya muda. Miungu haina msaada wowote zaidi ya kutufanya kuwa watumwa. Somo hili linatupatia changamoto ya kumrudia Mungu.

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 11/2025

Karibu katika mpango huu wa Soma Biblia Kila Siku mwezi wa Novemba. Utasoma kitabu cha Isaya. Utapata pia maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa na kutafakari Neno ulilosoma. Katika mpango huu, nukuu zote za Biblia zimenukuliwa kutoka katika Swahili Revised Union Version (SRUV).

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz