Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 11/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 11/2025

SIKU 20 YA 30

Watu wanapenda kuwatendea wenzao kile ambacho wao hawapendi kutendewa. Wanawatendea jirani zao hiana. Huu ni ubinafsi unaodai hali yako na kusahau ile ya wenzako. Hii si tabia ya Mungu, ambaye upendo ni asili yake. Ubinafsi unavunja ahadi, uaminifu na uhusiano miongoni mwa watu. Kutimiza ahadi, kutenda kwa uaminifu na kuimarisha uhusiano haviwezekani hadi awepo Kristo katikati yetu na hivyo katika taifa. Mwombe Mungu siku zote ili akuwezeshe kutenda kwa uaminifu bila kupoteza uhusiano naye.

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 11/2025

Karibu katika mpango huu wa Soma Biblia Kila Siku mwezi wa Novemba. Utasoma kitabu cha Isaya. Utapata pia maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa na kutafakari Neno ulilosoma. Katika mpango huu, nukuu zote za Biblia zimenukuliwa kutoka katika Swahili Revised Union Version (SRUV).

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz