Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 11/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 11/2025

SIKU 21 YA 30

Huu ni wito kutoka kwa Mungu. Watu wanaitwa waone na kushuhudia ukuu wa Mungu utokanao na kazi zake. Nabii anaweka bayana sifa za wale wote watakao na wanaoweza kuishi katika hali ya Mungu. Katika m.14 kuna swali:Ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto ulao; ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uteketezao milele?Zingatia jina katika m.15-16:Ni yeye aendaye kwa haki, anenaye maneno ya adili; ni yeye anayedharau faida ipatikanayo kwa dhuluma; akung'utaye mikono yake asipokee rushwa; azibaye masikio yake asisikie habari za damu; afumbaye macho yake asitazame uovu.Huyu ndiye atakayekaa juu; majabali ni ngome yake; atapewa chakula chake; maji yake hayatakoma. Wenye dhambi wanapaswa kuielewa hali yao mbele ya Mungu. Mwanadamu hawezi kuishi mbele ya Yesu akiwa na uovu wake. Mungu anafananishwa na moto ulao. Maisha ya ubadhirifu yanatuondolea sifa ya kukaa pamoja na Mungu Mtakatifu. Ukisamehewa uasi na dhambi zako unapata uhalali wa kuwa na Kristo.

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 11/2025

Karibu katika mpango huu wa Soma Biblia Kila Siku mwezi wa Novemba. Utasoma kitabu cha Isaya. Utapata pia maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa na kutafakari Neno ulilosoma. Katika mpango huu, nukuu zote za Biblia zimenukuliwa kutoka katika Swahili Revised Union Version (SRUV).

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz