Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 02/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 02/2025

SIKU 7 YA 28

Nyumba ya BWANA ilijengwa juu ya mlima. Siku za mwisho mlima huu utainuliwa juu ya milima mingine na kuwekwa imara. Ni mfano wa jinsi ufalme wa Mungu utakavyoshinda na kuwa mahali pa kukimbiliwa na mataifa yote kwa wingi. Ni matokeo ya jinsi Bwana Yesu alivyoinuliwa. Katika Yn 3:14 Yesu anaeleza mwenyewe kwambakama vileMusa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa. Tukimkimbilia ameahidi kwamba atatuonesha njia zake na kutufundisha kuzienda: Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; nitakushauri, jicho langu likikutazama(Zab 32:8). Neno lake litakuwa nuru yetu, na hukumu zake zitaleta amani katika jamii.

Andiko

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 02/2025

Soma Biblia Kila Siku 02/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Zaburi na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz