Soma Biblia Kila Siku 02/2025Mfano

Wanawake waliokaa Yerusalemu hawakukosa kitu chochote – isipokuwa kumcha BWANA. Isaya anaoneshwaBWANA atakavyowaondelea urembo wao mwingi na kuwaacha wakiwa uchi. Bwana atawapiga binti za Sayuni kwa pele za utosini, na Bwana ataifunua aibu yao(m.17). Badala ya marashi kutakuwa na uvundo. Waume wao pia hawatakuwepo tena. Watapigwa vitani, hadi wanawake saba watapigania kuolewa na mwanamume huyo huyo. Ni muhimu sana tujifunze kuikimbia hasira ya Mungu. Haiwezekani kwa kujaribu kumkimbia Mungu, bali kwa kumkimbilia. Tukiwa katika Kristo Yesu tuko salama, kwa sababuhakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu(Rum 8:1).
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 02/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Zaburi na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz