Soma Biblia Kila Siku 02/2025Mfano

BWANA atawaondolea watu wake vile vyote walivyotegemea na kuvitumainia. Ataondoa chakula, maji, n.k. Hakuna viongozi, maana ni nani atakaye kutawala palipobomoka? Wenyewe wamejiletea maangamizi haya.Kuonekana kwa nyuso zao kwashuhudia juu yao, wafunua dhambi yao kama Sodoma, hawaifichi. Ole wa nafsi zao, kwa maana wamejilipa nafsi zao uovu(m.9). Sababu ni kwamba wamempinga Mungu kwa maneno na matendo yao.Yerusalemu umebomolewa na Yuda wameanguka, kwa sababu ulimi wao na matendo yao ni kinyume cha Bwana, hata wayachukize macho ya utukufu wake(m.8). Waliyotenda yatawapata wao wenyewe:Mtu mbaya ... atapewa ijara ya mikono yake(m.11). Siku ile kuna kundi moja tu la watu ambao watakuwa heri. Ni wenye haki.Watakuwa heri, kwa maana watakula matunda ya matendo yaowaliyoyatenda katika Bwana (m.10). Watakula matunda hayo wakijua kwamba hata hayo yote yatokana na upendo wa Mungu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 02/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Zaburi na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz