Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 02/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 02/2025

SIKU 6 YA 28

“Mji huu” ni Yerusalemu, tena ni mfano wa watu wa Mungu. Walikuwa waaminifu kwa BWANA, lakini wakamwacha, wakawa makahaba wa kiroho wanaoabudu miungu (chini ya mialoni ile inayotajwa katika m.29). Sasa mji umejaa ufisadi na uonevu mwingi. BWANA ametoa wito wajitakase:Ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya(m.16). Lakini wameshindwa, au hata wamekataa. Sasa anatangaza kwamba yeye mwenyewe atarejesha utakatifu na kuikomboa Sayuni. Unabii wa Isaya unatimia katika Injili ya Mathayo kupitia Ukombozi aliuoleta Yesu. Linganisha Bwana anavyosema katika m.27 na anavyosema kuhusu “mtumishi” wake, ambaye ni Yesu, katika Mt 12:18-21:Sayuni itakombolewa kwa hukumu, na waongofu wake kwa haki(m.27).Nitatia roho yangu juu yake, Naye atawatangazia Mataifa hukumu. Hatateta wala hatapaza sauti yake; Wala mtu hatasikia sauti yake njiani. Mwanzi uliopondeka hatauvunja, Wala utambi utokao moshi hatauzima, Hata ailetapo hukumu ikashinda. Na jina lake Mataifa watalitumainia(Mt 12:18-21). Ila wasiokubali, Mungu anawaambia kwamba watatupwa nje kama takataka:Nitakuelekezea wewe mkono wangu, na kukutakasa takataka zako kabisa, na kukuondolea bati lako lote(m.25).

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 02/2025

Soma Biblia Kila Siku 02/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Zaburi na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz