Soma Biblia Kila Siku 02/2025Mfano

Ujumbe wa somo ni wazi: Ipo siku ambapomajivuno ya mwanadamu yatainamishwa ... naye BWANA, yeye peke yake, atatukuzwa(m.17). Itakuwa siku ya kutisha kwa wote wanaoshikamana na kiburi chao. Basi, tusimwamini binadamu, haijalishi kama ni watu wengine au sisi wenyewe, maana uhai wetu ni kama pumzi, haudumu. Ndivyo tunavyokumbushwa katika m.22: Pumzi yake [mwanadamu] i katika mianzi ya pua yake. Huo ni wito wa toba. Nyumba ya Israeli wanaaswa kurudi na kuenenda katika nuru ya BWANA:Enyi wa nyumba ya Israeli, njoni, twende katika nuru ya Bwana.Sisi pia tumepewa wito huu.Maana yake inafafanuliwa zaidi katika 1 Yoh 1:5-7: Tukisema ya kwamba twashirikiana naye, tena tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatuifanyi iliyo kweli; bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote. Jihoji kama unaishi na kutembea katika nuru?
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 02/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Zaburi na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz