Soma Biblia Kila Siku 02/2025Mfano

“Mabaki” wana hali tofauti sana na wale waliohukumiwa na Mungu katika ml.3. Siri ya tofauti hiyo ni “chipukizi la BWANA”. Yer 23:5 unaeleza hilo ni mfano wa Bwana Yesu, maana hapo Bwana asema:Tazama siku zinakuja, nitakapomchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye atamiliki mfalme, atatenda kwa hekima, naye atafanya kuhumu na haki katika nchi. Atawaletea hao waliobaki wokovu kwa njia ya kuwasafisha na uchafu wa dhambi. Wenyewe watajisikia kama kupitishwa kwenye hukumu na uteketezaji, Roho wake akiwasafisha kama fedha na kuwatakasa. Lakini tokeo lake ni jema sana: watakuwa watakatifu.Yeye aliyebaki katika Sayuni, na yeye aliyeachwa ndani ya Yerusalemu, ataitwa mtakatifu; yaani, kila mmoja aliyeandikwa miongoni mwa hao walio hai ndani ya Yerusalemu; hapo Bwana atakapokuwa ameuosha uchafu wa hao binti za Sayuni na kuisafisha damu ya Yerusalemu kati yake, kwa roho ya hukumu na kwa roho ya kuteketeza(m.3-4). Wote wampokeao Yesu ni matunda ya kazi yake, na kimbilio lao ni kwake.Kutakuwa na hema kuwa uvuli wakati wa mchana kwa sababu ya hari, na kuwa mahali pa kukimbilia na kujificha wakati wa tufani na mvua(m.6).
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 02/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Zaburi na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz