Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 02/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 02/2025

SIKU 12 YA 28

Wimbo wa shamba la mizabibu una ujumbe mzito. Mpenzi wa Isaya ni Mungu, na shamba ni mfano wa “nyumba ya Israeli” (m.7), yaani watu wake. Shamba lilikuwa mahali pazuri sana lililolimwa na kuwekewa ulinzi mzuri. Kwa hiyo baadhi ya Wayuda walifanikiwa sana kimwili. Lakini kiroho walizaa zabibu-mwitu tu! Je, ipo tofauti leo? Tafakari swali hili kwa kulinganisha siku hizi na m.8:Ole wao waongezao nyumba baada ya nyumba, na kuweka shamba karibu na shamba, hata hapana nafasi tena. Katika m.5-6 Mungu anatangaza atakalofanya:Nitaliharibushamba! Kusudi lake ni hili:Mwanadamu atashushwa,lakini Bwana atatukuzwa kwa ajili ya haki yake.Katika m.15-16 imefafanuliwa hivi:Mtu mnyonge ainamishwa, na mtu mkubwa amedhilika, na macho yao walioinuka hunyenyekezwa, bali Bwana wa majeshi ametukuzwa katika hukumu, na Mungu aliye Mtakatifu ametakswa katika haki.

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 02/2025

Soma Biblia Kila Siku 02/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Zaburi na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz