Soma Biblia Kila Siku 02/2025Mfano

M.23-25 inatukumbusha kwamba kwa kawaida jeuri dhidi ya Mungu hutupelekea kwenye maangamizi:Mahali palipokuwa na mizabibu elfu, iliyopata fedha elfu, patakuwa mahali pa mbigili na miiba tu. Mtu atakayekwenda huko atakwenda na mishale na upinde; kwa sababu nchi yote itakuwa ina mibigili na miiba. Na vilima vyote vilivyolimwa kwa jembe, hutafika huko kwa sababu ya kuiogopa mibigili na miiba, lakini hapo patakuwa mahali pa kupeleka ng'ombe, mahali pa kukanyagwa na kondoo. Lakini kumcha Mungu hutupa maarifa na hekima ya kweli pamoja na kupokea baraka na uzima wa milele. Basi tuishi tukijua kwamba tukidharau maonyo na mafundisho ya Mungu kwa kufuata hekima zetu wenyewe, tutakuwa tunajiandalia mazingira magumu ya maisha ya sasa na ya baadaye. Lakini tukiishi kwa kumsikiliza, kumpenda na kumtii Roho wa Mungu tutakuwa tunakirimiwa furaha na amani ya sasa na ya baadaye.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 02/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Zaburi na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz