Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 02/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 02/2025

SIKU 17 YA 28

Mwaka 731 KK Ahazi alikuwa mfalme wa Yuda. Alianza kutawala akiwa na umri wa miaka ishirini hivi. Ahazi alimwacha Bwana akafuata miungu mingine.Akatawala miaka kumi na sita katika Yerusalemu; wala hakufanya mema machoni pa Bwana Mungu wake, kama Daudi babaye. Lakini aliiendea njia ya wafalme wa Israeli, hata akampitisha mwanawe motoni, sawasawa na machukizo ya mataifa Bwana aliowafukuza mbele ya wana wa Israeli. Kisha akatoa sadaka na kufukiza uvumba katika mahali pa juu, na juu ya vilima, na chini ya kila mti mbichi(2 Fal 16:2-4). Ndipo Isaya anatumwa kumwonya. (Soma mwenyewe m.3-9.) Mungu anaahidi kumpa ishara ya ukombozi. Yamhusu Yesu.Bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli(m.14). Ahazi anakataa. Siye mfano wa kuigwa na wazazi, walezi wala viongozi wa jamii, maana tabia za Ahazi ni chukizo kwa Bwana Mungu. Sisi tulio wana wa Mungu tunapaswa kumheshimu na kufuata yaliyo mapenzi ya Mungu tu, na siyo miungu mingine.

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 02/2025

Soma Biblia Kila Siku 02/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Zaburi na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz