Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 02/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 02/2025

SIKU 16 YA 28

Ee Bwana, hata lini?(m.11). Je, unaelewa swali la Isaya? Anapoitikia wito wa BWANA, anatumwa kupeleka ujumbe mkali. Watu hudai wanasikia na kuona, lakini ufahamu uletao kurejea na kuponywa haupo, na inabidi Isaya awaambie:Fulizeni kusikia, lakini msifahamu; fulizeni kutazama, lakini msione. Uunoneshe moyo wa watu hawa, ukayatie uzito masikio yao, ukayafumbe macho yao; wasije wakaona kwa macho yao, na kusikia kwa masikio yao, na kufahamu kwa mioyo yao, na kurejea na kuponywa(m.9-10). Hali itazidi kuwa mbaya. Nchi itakuwa mahame, hamna kitu kitakachobaki. Isipokuwa kisiki! Maana ya m.13 ni kwambakisiki hicho ni mbegu takatifu ya chanzo kipya(Biblia Habari Njema). Kutatokea chipukizi katika kisiki hicho.Litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda(11:1). Mungu atamtuma Kristo. Dunia itakuwa tena ufalme wa Mungu.

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 02/2025

Soma Biblia Kila Siku 02/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Zaburi na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz