Soma Biblia Kila Siku 02/2025Mfano

Mwaka alipokufa Uzia, Isaya alipewa maono ya utukufu wa Bwana, maono ya kutisha kwa mwenye dhambi. Lazima afe, isipokuwa Mungu mwenyewe akiingia kati na kuondoa uovu huu unaoambatana nasi sote. Kwamba dhambi yake Isaya “imefunikwa” (m.7), maana yake siyo kwamba ingeweza kufunuliwa tena. Upatanisho ulipofanyika, dhambi haipo tena. Huo unamwezesha Isaya kusikia wito wa Mungu na kumtilia ujasiri wa kujibu kwamba yuko tayari kumtii. Mungu amtume kokote apendavyo. Je, umesikia wito wa Mungu kwako?
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 02/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Zaburi na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz