Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 02/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 02/2025

SIKU 14 YA 28

Watu walisema nuru ya Bwana ni giza na kulisifu giza lao wenyewe kuwa nuru. Jibu la Mungu kwao ni wazi:Ole wao wasemao kwamba uovu ni wema, na kwamba wema ni uovu; watiao giza badala ya nuru, na nuru badala ya giza; watiao uchungu badala ya utamu, na utamu badala ya uchungu(m.20)!Sasa hiyo nuru yao itatiwa giza na Mungu. Hasira ya BWANA itawaka juu ya watu wake kwa jinsi walivyolidharau neno lake. Mwenyewe atawaita watu fulani watekeleze hukumu yake. Hakuna atakayeweza kuwapinga wala kuleta wokovu. Nchi itagubikwa giza na dhiki. Hukumu hii ya Mungu ni kama kukata mti hadi kibaki kisiki tu. Hata kama kunasehemu moja katika sehemu kumi ndani ya [nchi], italiwa hii nayo; kama mvinje na kama mwaloni, ambao shina lake limebaki (6:13). Lakini zingatia pia mstari huu unavyoendelea kusema:Ingawa imekatwa; kadhalika mbegu takatifu ndiyo shina lake. Katika Biblia Habari Njema neno hili limetafsiriwa hivi:Kisiki hicho ni mbegu takatifu ya chanzo kipya. Kristo ndiye chanzo hicho.

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 02/2025

Soma Biblia Kila Siku 02/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Zaburi na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz