1
Mateo 7:7
Swahili Roehl Bible 1937
SRB37
Ombeni! ndipo, mtakapopewa. Tafuteni! ndipo, mtakapoona. Pigeni hodi! ndipo, mtakapofunguliwa mlango.
Linganisha
Chunguza Mateo 7:7
2
Mateo 7:8
Kwani kila anayeomba hupewa, naye anayetafuta huona, naye anayepiga hodi hufunguliwa mlango.
Chunguza Mateo 7:8
3
Mateo 7:24
*Basi, kila mtu anayeyasikia haya maneno yangu na kuyafanyiza atafanana na mtu mwenye akili aliyeijenga nyumba yake mwambani.
Chunguza Mateo 7:24
4
Mateo 7:12
Yo yote, mnayotaka, watu wawafanyie ninyi, nanyi mwafanyie yaleyale! Kwani hayo ndiyo Maonyo na Wafumbuaji.
Chunguza Mateo 7:12
5
Mateo 7:14
Tena uko mlango ulio mfinyu, nayo njia yake inasonga; ndiyo inayokwenda penye uzima, lakini wanaoiona ni wachache.
Chunguza Mateo 7:14
6
Mateo 7:13
*Uingieni mlango ulio mfinyu! Kwani liko lango lililo pana, nayo njia yake ni kubwa; ndiyo inayokwenda penye kuangamizwa, nao wanaoingia mle ni wengi.
Chunguza Mateo 7:13
7
Mateo 7:11
Basi, ninyi mlio wabaya mkijua kuwapa watoto wenu vipaji vyema, Baba yenu alioko mbinguni asizidi kuwapa mema wanaomwomba?
Chunguza Mateo 7:11
8
Mateo 7:1-2
Msiumbue mtu, msije mkaumbuliwa! Kwani kama mnavyowaumbua wengine, ndivyo, mtakavyoumbuliwa wenyewe. Kipimo, mnachopimia wengine, ndicho, mtakachopimiwa nanyi.
Chunguza Mateo 7:1-2
9
Mateo 7:26
Lakini kila mtu anayeyasikia haya maneno yangu asipoyafanyiza atafanana na mtu mpumbavu aliyeijenga nyumba yake mchangani.
Chunguza Mateo 7:26
10
Mateo 7:3-4
Nawe unakitazamiani kibanzi kilichomo jichoni mwa ndugu yako, lakini gogo lililomo jichoni mwako wewe hulioni? Au utamwambiaje ndugu yako: Ngoja, nikitoe kibanzi katika jicho lako, wewe mwenyewe ukiwa unalo gogo zima jichoni mwako?
Chunguza Mateo 7:3-4
11
Mateo 7:15-16
Jilindeni kwa ajili ya wafumbuaji wa uwongo! Wanawajia wamevaa kama kondoo, lakini mioyoni ni mbwa wa mwitu wenye ukali. Kwa matunda yao mtawatambua. Je? Huchuma zabibu miibani? Au huchuma kuyu mikongeni?
Chunguza Mateo 7:15-16
12
Mateo 7:17
Hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; lakini mti mwovu huzaa matunda mabaya.
Chunguza Mateo 7:17
13
Mateo 7:18
Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu hauwezi kuzaa matunda mazuri
Chunguza Mateo 7:18
14
Mateo 7:19
Kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa, utupwe motoni.
Chunguza Mateo 7:19
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video