Soma Biblia Kila Siku 06/2024Sample

Anayestahili kupokea sifa na utukufu ni Mungu peke yake. Lakini mara nyingi tumekuwa tukiangalia tunachoweza kukipatasisi, badala ya kutafuta kumpa Mungu zile sifa anazostahili. Kwa namna hiyo tunashindwa kama Gehazi. Nabii Elisha alikataa kupokea zawadi yoyote,akasema, Kama Bwana aishivyo, ambaye nimesimama mbele yake, sipokei kitu. Akamshurutisha apokee; lakini akakataa(m.16). Ni alama ya kweli ya mtu wa Mungu kwamba hayuko kwa ajili ya kutafuta masilahi yake, bali hutafuta ustawi wa wengine. Kwa mfano, ndivyo alivyoishi Paulo. Alipoagana na Wakristo huko Mileto alisema,Sikutamani fedha wala dhahabu, wala mavazi ya mtu. Ninyi wenyewe mnajua ya kuwa mikono yangu hii imetumika kwa mahitaji yangu na ya wale waliokuwa pamoja nami. Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea(Mdo 20:33-35). Hebu tuishi ili watu wauone utukufu wa Mungu na kumwamini yeye pekee.
Scripture
About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 06/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa sita pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Timotheo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Related Plans

Who Am I, Really? Discovering the You God Had in Mind

Overcoming the Trap of Self-Pity

Am I Really a Christian?

Drive Time Devotions - Philippians

Positive and Encouraging Thoughts for Women: A 5-Day Devotional From K-LOVE

16 Characteristics of the God-Kind of Love - 1 Corinthians 13:4-8

Faith @ Work

Reimagine Influence Through the Life of Lydia

Faith in Trials!
