YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 02/2024Sample

Soma Biblia Kila Siku 02/2024

DAY 7 OF 29

Taifa linahitaji mwongozo wa namna ya watu kutendeana. Hakuna mtu anayestahili kuwa mtumwa katika maisha yake yote. Kuna mwaka wa kuachiwa huru. Ndio mwaka wa Jubilii. Sheria hizi zimewekwa ili tujue kuwa kila tutendalo lina matokeo yake. Watu wa Mungu wanapaswa kuishi kwa kuwajibika, hasa kuzingatia jinsi tunavyokusudia kuwatendea wengine. Kuishi kwa kuwajibika ni kuwatendea kwa haki watu wote. Tukumbuke kuwa wameumbwa kwa mfano wa Mungu. Kuwa mnyonge hakuhalalishi kunyanyaswa.Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii(Mt 7:12).

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 02/2024

Soma Biblia Kila Siku 02/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu

More