Soma Biblia Kila Siku 02/2024Sample

Mungu wetu ni Mungu aliye hai. Ni Mungu anayewasiliana na wanadamu. Ni Mungu aliye tofauti na miungu isiyosema wala kujitambulisha kwa watu. Mungu wa kweli anatoa utaratibu wa jinsi ya kuhusiana naye kwa ibada. Musa alisimama kati ya Mungu na taifa la Israeli. Mungu na taifa walikutana kupitia kwa Musa. Lakini wakati huu wa sasa, ambao ni wakati wa Agano Jipya, Mungu anasema na sisi moja kwa moja kwa njia ya Mwana wake, Yesu Kristo.Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi,mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.Yeye kwa kuwa ni mng'ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu(Ebr 1:1-3). Tafakari maana yake kwake, kisha umshukuru Mungu kwa neema hii.
Scripture
About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 02/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Related Plans

Run With Endurance: Faith and Perseverance for Everyone

Keep Standing: When the Weight Feels Heavy

A Heart Prepared for Thanksgiving

Faith That Feels Real: Part 4 - Trusting God in the Hardest Times

Reset and Recenter: A Christian's Guide to Faith and Technology

Believing Without Seeing

30 Scripture Based Prayers for Your Marriage

Friendship With Jesus

Prayer
