Soma Biblia Kila Siku 02/2024Sample

Fungu hili linaleta amri kumi za Mungu. Amri hizi zinagawanyika katika mafungu makuu mawili. Amri za 1-3 zinahusu uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu. Ni uhusiano baina ya Mwumbaji na kiumbe wake. Kwa vyovyote vile ukizishika vema amri za Mungu unapata mwongozo wa jinsi ya kuhusiana na wanadamu wenzako. Yesu Kristo anajumlisha amri hizi kwa kusema kuwa amri kuu kuliko zote ni Upendo. Ndiyo amri ya kumpenda Mungu na jirani zetu. Tafakari Yesu anavyosema katika Mk 12:29-31,Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja; nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.
Scripture
About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 02/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Related Plans

Run With Endurance: Faith and Perseverance for Everyone

Keep Standing: When the Weight Feels Heavy

A Heart Prepared for Thanksgiving

Faith That Feels Real: Part 4 - Trusting God in the Hardest Times

Reset and Recenter: A Christian's Guide to Faith and Technology

Believing Without Seeing

30 Scripture Based Prayers for Your Marriage

Friendship With Jesus

Prayer
