Soma Biblia Kila Siku 02/2024Sample

Kwa nini watu waliambiwa hawawezi kumwona Mungu? Ni kwa sababu Mungu ni mtakatifu na sisi ni wenye dhambi. Wanadamu walipoteza utukufu wa kuonana na Mungu na kukaa karibu naye pale walipovunja amri ya Mungu katika bustani ya Edeni.Kwa hiyo Bwana Mungu akamtoa katika bustani ya Edeni, ailime ardhi ambayo katika hiyo alitwaliwa.Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima(Mwa 3:23-24). Kuja kwa Yesu kumeondoa wingu lililokuwa linazuia tusiuone uso wa Mungu Mtakatifu. Damu ya Yesu ndiyo inayoleta utakaso unaodumu. Bila kutakaswa kwa damu hiyo hakuna uwezekano wa kukutana na Mungu. Damu ya Yesu inatosha kutupeleka katika wokovu wa kweli.
Scripture
About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 02/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Related Plans

Run With Endurance: Faith and Perseverance for Everyone

Keep Standing: When the Weight Feels Heavy

A Heart Prepared for Thanksgiving

Faith That Feels Real: Part 4 - Trusting God in the Hardest Times

Reset and Recenter: A Christian's Guide to Faith and Technology

Believing Without Seeing

30 Scripture Based Prayers for Your Marriage

Friendship With Jesus

Prayer
