Soma Biblia Kila Siku Julai/2022Sample

Kumbe, Mungu ndiye aliyewafanya watu wake wawe mateka. Sasa anawaita wakimbilie Yerusalemu. Kuna makusudi mahususi ya kuruhusu watekwe kwanza, kisha kuwakusanya tena: Mataifa yote wajue ukuu wa Bwana. Ni Mungu wa misheni. Atakalofanya ni tendo la kiutume. Ujumbe wake unawahusu watekaji na watekwaji. Anasema, Tazama, nitatikisa mkono wangu juu yao, nao watakuwa mateka ya hao waliowatumikia; nanyi mtajua ya kuwa Bwana wa majeshi amenituma. Imba, ufurahi, Ee binti Sayuni; maana, tazama, ninakuja, nami nitakaa kati yako, asema Bwana (m.9-10). Tendo hili liwavute hata mataifa ili mwamini Mungu. Mwokozi ni wa wote (m.11, Mataifa mengi watajiunga na Bwana katika siku ile, nao watakuwa watu wangu). Anataka mataifa yote watiishwe chini yake. Mbele ya Mungu hakuna tukio lisilokuwa na la kutufundisha.
Scripture
About this Plan

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Julai pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Zakaria na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Related Plans

Game Changers: Devotions for Families Who Play Different (Age 8-12)

Legacy Lessons W/Vance K. Jackson

Awakening Faith: Hope From the Global Church

Protocols, Postures and Power of Thanksgiving

Rebuilt Faith

God's Book: An Honest Look at the Bible's Toughest Topics

30 Powerful Prayers for Your Child Every Day This School Year

24 Days to Reflect on God's Heart for Redemption

You Say You Believe, but Do You Obey?
