Soma Biblia Kila Siku Julai/2022Sample

Ujumbe wa Mungu unahusu Yerusalemu mpya. Mtu mwenye kamba anataka kupima ukubwa wa ujenzi wa kuta zake, lakini kazi hiyo haitahitajika. Sababu moja ni mji wa Mungu kuenea sana kutokana na kukaliwa na watu wengi. Lakini sababu kuu ni ahadi ya ulinzi utakaowekwa na Mungu. Yeye mwenyewe ndiye ule ‘ukuta’ utakaolinda taifa lake: Kwa maana mimi, asema BWANA, nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka pande zote, nami nitakuwa huo utukufu ndani yake (m.5). Tafakari jambo hili zaidi ukilinganisha na maneno yafuatayo: Mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-Kondoo (Ufu 21:23). Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani? (Zab 27:1)
Scripture
About this Plan

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Julai pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Zakaria na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Related Plans

Game Changers: Devotions for Families Who Play Different (Age 8-12)

Legacy Lessons W/Vance K. Jackson

Awakening Faith: Hope From the Global Church

Protocols, Postures and Power of Thanksgiving

Rebuilt Faith

God's Book: An Honest Look at the Bible's Toughest Topics

30 Powerful Prayers for Your Child Every Day This School Year

24 Days to Reflect on God's Heart for Redemption

You Say You Believe, but Do You Obey?
