YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022Sample

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022

DAY 9 OF 30

Huduma ya Injili yahitaji watendaji waaminifu na wasioangalia mambo yao wenyewe. Tena yahitaji watu wanaopenda kuwatumikia wengine kwa bidii, hata kama miili yao itaumia na kuteseka. Tangu wakati wa Paulo wengi wamependa kuhudumu panapo maslahi mazuri na raha za kijamii. Injili haitastawi namna hii. Ni wapi Mungu amekutuma lakini unasita kwa sababu maslahi ni haba? Mkabidhi Mungu na utii, ukitafuta vya Kristo.

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Juni pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wafilipi na Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More