YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022Sample

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022

DAY 13 OF 30

Tuwapo duniani tutambue kuwa tu wasafiri. Uwenyeji wetu uko mbinguni. Tujihadhari na watu watafutao kujinufaisha kwa mafundisho yapotoshayo. Sisi twajua Kristo yuko mbinguni ambako atatupeleka atakapotujia mara ya pili, tukaishi naye tukiwa na miili mipya ya utukufu, ambayo atatuvika kwa uweza wake mkuu. Basi na tufuate mfano wa Paulo ili tusikose kuwa na Bwana wetu Yesu Kristo aliyetununua kwa kifo chake, na akawa mshindi wa mauti kwa ajili yetu.

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Juni pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wafilipi na Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More