YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021Sample

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021

DAY 7 OF 30

Maana ya m.1 ni kuja kwa Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste. Tukio la Yesu kugeuka sura mlimani linathibitisha kwa njia tatu kwamba yeye kweli ni Mwana wa Mungu aliyetumwa duniani kwa kazi ya ukombozi: 1. Aligeuka sura, na utukufu wake wa kimungu ukaonekana (m.2b-3: akageuka sura yake mbele yao; mavazi yake yakimeta-meta, meupe mno, jinsi asivyoweza dobi duniani kuyafanya meupe). 2. Manabii wawili walioko Mbinguni wakaonekana pamoja naye (m.4). Walizungumzia nini? Jibu linapatikana katika Lk 9:31, Wakanena habari za kufariki kwake atakakotimiza Yerusalemu. 3. Sauti ya Mungu ikasikika kama wakati wa ubatizo wa Yesu, ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, msikieni yeye (m.7). Je, umelifuata agizo la Mungu la kumsikia na kumtii Yesu Kristo?

Scripture

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More