Soma Biblia Kila Siku Juni 2021Sample

Hamkumbuki (m.18)? Wanafunzi walikuwa wameona miujiza mikubwa wakati Yesu alipowashibisha maelfu ya watu. Sasa wako chomboni wakiwa na mkate mmoja tu. Wakasumbukia jambo hili, tena wakabishana. Ni kana kwamba wamesahau yote yaliyopita. Ni wazito kuamini uwezo wa Yesu. Na Yesu akawalaumu. Hata sisi Wakristo wa siku hizi ni wepesi kusahau. Bila shaka kila mmoja wetu angeweza kusimulia jinsi Mungu alivyowahi kumsaidia. Na Yesu hajabadilika. Bado ni yeye yule. Tukumbushane! Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, Wala usizisahau fadhili zake zote (Zab 103:2).
Scripture
About this Plan

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Related Plans

Everyday Prayers for Christmas

The Holy Spirit: God Among Us

Sharing Your Faith in the Workplace

Simon Peter's Journey: 'Grace in Failure' (Part 1)

Reimagine Influence Through the Life of Lydia

Positive and Encouraging Thoughts for Women: A 5-Day Devotional From K-LOVE

Never Alone

Gospel-Based Conversations to Have With Your Preteen

The Bible in a Month
