Soma Biblia Kila Siku Juni 2021Sample

Mambolezo yanaendelea. Licha ya uzuri na heshima alizojichumia mfalme wa Tiro kutokana na wafanyabiashara aliochuuza nao, mahusiano hayo yameleta udhalimu pia, na uovu (m.18a: Kwa wingi wa maovu yako, katika uovu wa uchuuzi wako, umepatia unajisi patakatifu pako). Hakika Mungu atatekeleza hukumu yake juu ya dhambi zake. Na Mungu akishajitukuza hivyo, atakusanya Israeli tena na kurudisha watu wake wakae salama. Bwana MUNGU asema hivi; Nitakapokuwa nimewakusanya nyumba ya Israeli, na kuwatoa katika watu ambao wametawanyika kati yao, na kutakasika kati yao machoni pa mataifa, ndipo watakapokaa katika nchi yao wenyewe, niliyompa mtumishi wangu, Yakobo. Nao watakaa humo salama; naam, watajenga nyumba, na kupanda mashamba ya mizabibu, na kukaa salama; nitakapokuwa nimetekeleza hukumu zangu juu ya watu wote, wanaowatenda mambo ya jeuri pande zote; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wao (m.25-26). Matendo yote ya Mungu, ya hukumu na wokovu, yana lengo moja: Nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana MUNGU (m.22,23,24) - Mungu wao (= Israeli; m.26).
Scripture
About this Plan

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Related Plans

Reimagine Transformation Through the Life of Paul

House of David, Season 2: Trusting God in the Middle of the Story

Faith in Action: A Journey Through James

How to Love Your Work and God

The Letter to the Philippians

Lighting Up Our City Video 2: Avoiding Insider Language

How Is It With Your Soul?

Honest to God

How to Love Like Jesus
