YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021Sample

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021

DAY 23 OF 30

Hukumu ya Mungu juu ya Misri itafanyika kwa kutumia jeshi la Babeli, kama anavyosema mwenyewe katika m.10: Nitaukomesha wingi wa watu wa Misri, kwa mkono wa Nebukadreza, mfalme wa Babeli. Jeshi hili lilitumika kuadhibu Tiro na kutawala mji huu miaka 13, bila malipo yoyote. Mungu anaonyesha haki zake hata kwa taifa lisilomjua. Jeshi hili linalipwa kwa kuruhusu kuiharibu kabisa Misri. Mungu haonyeshi huruma kwa yeyote mwenye kiburi. Adhabu yake itaonyesha kwamba yeye ndiye Bwana. Lakini Mungu ana shauku kubwa ya kufadhili pia. Zingatia ahadi yake katika m.21: Siku ile nitawachipushia nyumba ya Israeli pembe. “Pembe” ni mfano wa wokovu na ukombozi.

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More