Soma Biblia Kila Siku Juni 2021Sample

Eze 31 hukumbusha anguko la Ashuru mwaka 612 k.K. Miaka 25 imekwenda, lakini kiburi cha Misri kiko palepale. Basi, katika 32:1 Mungu anaamuru maombolezo juu ya Misri. Watu wengi watashangazwa kwa jinsi Misri itafanywa ukiwa na kuangushwa (m.10: Nami nitawashangaza watu wa kabila nyingi kwa habari zako, na wafalme wao wataogopa sana kwa ajili yako, nitakapoutikisa upanga wangu mbele yao; nao watatetemeka kila dakika, kila mtu kwa ajili ya uhai wake, katika siku ya kuanguka kwako). Kwa nini watatemeka kwa ajili ya uhai wao? Kwa sababu walitegemea nguvu ileile ya Misri! Vipi na sisi Wakristo? Je, tumeingiwa na upofu hata tusione maonyo ya Mungu juu ya kibuti na kutegemea nguvu ya kibinadamu? Tujichunguze mioyo yetu!
Scripture
About this Plan

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Related Plans

Every Thought Captive

3 - LORD'S PRAYER - the Lord´s Requirements

As He Purposeth in His Heart by Vance K. Jackson

The Origin of Our Story

Don’t Know What You’re Doing After Graduation? Good.

The Rapture of the Church

Philippians - Life in Jesus

UNPACK This...Being a Good Teammate in Life

Seasons of Hardship: Live the Jesus Way
