YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021Sample

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021

DAY 18 OF 30

Somo hili linaanza mfululizo wa hukumu juu ya Tiro (hadi 29:19; Tiro ni sehemu ya Lebanoni ya leo). Mji huu wa bandari kwenye Bahari ya Kati ulikuwa muhimu sana kwa biashara. Wakazi walijigamba kwa furaha kuwa na umaarufu zaidi baada ya Yerusalemu kuangushwa. Tiro amesema juu ya Yerusalemu, Aha! Yeye amevunjika aliyekuwa lango la kabila za watu; amenigeukia; nitajazwa kwa kuwa sasa ameharibika (m.2). Kwa hiyo Mungu anakasirika na kutangaza hukumu za aina mbalimbali. Kujiinua kwa mtu yeyote ni kuandaa anguko lake mwenyewe, kama m.15-21 inavyotukumbusha. Tujihadhari na kiburi na kuhukumu watu wa Mungu, kwani matokeo yake ni ya kutisha. Nitakufanya kuwa kitu cha kutisha, wala hutakuwako tena; ujapotafutwa, lakini hutaonekana tena kabisa, asema Bwana MUNGU (m.21).

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More