Soma Biblia Kila Siku Juni 2021Sample

Katika Eze 25-32 kuna hukumu saba juu ya mataifa yaliyo kinyume na taifa teule la Mungu. Somo la leo linaonyesha hukumu juu ya Amoni (m.3), Moabu na Seiri (m.8), Edomu (m.12) na Wafilisti (m.15). Sababu za hukumu ni kucheka kwa dharau, kufikiria Israeli ni sawa na wao tu, na kulipiza kisasi kwa ujeuri. Tutambue kuwa Mungu ndiye pekee mwenye maamuzi ya mwisho juu ya watu wake. Agano lake li imara na upendo wake haupungui kwa watu wake. Maana milima itaondoka, na vilima vitaondolewa; bali wema wangu hautaondoka kwako, wala agano langu la amani halitaondolewa; asema Bwana akurehemuye (Isa 54:10). Sisi tunaomwamini Yesu, Mungu wetu ni huyohuyo!
Scripture
About this Plan

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Related Plans

Everyday Prayers for Christmas

The Holy Spirit: God Among Us

Sharing Your Faith in the Workplace

Simon Peter's Journey: 'Grace in Failure' (Part 1)

Reimagine Influence Through the Life of Lydia

Positive and Encouraging Thoughts for Women: A 5-Day Devotional From K-LOVE

Never Alone

Gospel-Based Conversations to Have With Your Preteen

The Bible in a Month
