YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Machi 2021Sample

Soma Biblia Kila Siku Machi 2021

DAY 5 OF 31

Katika huduma ya Injili ni muhimu kujua mazingira ya wale ambao unahusiana nao. Zingatia mahitaji na mambo yao, na angalia nafasi ya kuwashuhudia Injili. Usijifanye unajua kila kitu, bali uwafanye wengine wajisikie kuwa wamepokelewa na kukubalika. Lengo ni kumtukuza Mungu na kuwaleta watu kwa Kristo. Ndiko kuwa tayari kuishi popote, wakati wowote na kwa watu wote bila kubagua. Ndivyo tunavyojifunza kwa Kristo na Paulo mfuasi wake. Je, u tayari wewe kutumika kuwaleta watu kwa Kristo?