YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Machi 2021Sample

Soma Biblia Kila Siku Machi 2021

DAY 31 OF 31

Desturi na matakwa ya wenye karama viligongana na maagizo ya Bwana. Paulo anatoa utaratibu kwa ibada za kiusharikakanisani ili uhuru wa Injili usilete fujo, na Wakristo wasivunje neno la Bwana juu ya ni nani anayetakiwa kuwa kichwa (11:3, Kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu). Kule Korintho mwanamke hakupewa elimu ya dini. Mungu ataka ajifunze, na ajifunzekatika utulivu(1 Tim 2:11). Wanawake wanazo karama za Roho na kutumiwa na Mungu katika kumshuhudia hata mahali ambapo wanaume hawawezi kupafikia. Vema! Wasivunje tu utaratibu huo uliowekwa na Mungu.