YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Machi 2021Sample

Soma Biblia Kila Siku Machi 2021

DAY 4 OF 31

Paulo alistahili kupata riziki zake kutokana na kazi yake: Bwana ... ameamuru kwamba wale waihubirio Injili wapate riziki kwa hiyo Injili(m.14). Hata hivyo aliihubiri Injili bila kudai haki zake kwa Wakristo wa Korintho. Mahitaji yake ya kidunia alijipatia kwa kushona hema. Ni kwa sababu Paulo aliongozwa na nia ya Mungu iliyokuwa ndani yake. Kuihubiri Injili ilikuwa ni kipawa na wito wake, na Paulo alitumia karama zake zote kwa ajili ya kuieneza. Ni karama gani ambazo Mungu amekupatia wewe? Je, unazitumia kama Paulo kwa ajili ya kumheshimu na kumtumikia Mungu?