YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Machi 2021Sample

Soma Biblia Kila Siku Machi 2021

DAY 8 OF 31

Waisraeli kuvuka kutoka Misri kwenda ng’ambo ya bahari ndiko kubatizwa kwao katika Musa. Tendo hili ni mfano wa Mungu anavyotuokoa kutoka dhambini, akituunganisha katika ubatizo wa Kikristo tuwe mali ya Kristo. Aliyebatizwa aishi Kikristo akiongozwa na Kristo kama wingu lilivyowaongoza Waisraeli. Kristo ndiye mwamba. Kutoka kwake twapata maji yaliyo hai, na mana ni alama ya Chakula cha Bwana. Tule na kunywa, na tumfuate Kristo ili tusiangamizwe kama Waisraeli wengi, bali tufike nchi ya ahadi.