YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Machi 2021Sample

Soma Biblia Kila Siku Machi 2021

DAY 6 OF 31

Anayeshuhudia Injili awe mfano wa kuigwa. Paulo anaeleza tabia ya Mkristo akitumia mfano wa mwanariadha. Ili kushinda shindano lolote ni lazima tuwe na nidhamu. Mafanikio yoyote huambatana na nidhamu. Tabia ya kujikana huleta mafanikio ya mwili, akili na roho. Ndivyo maisha kwa ujumla wake yalivyo. Wokovu tunao tayari. Tunakimbia ili tusiupoteze njiani. Maombi, ibada, na kujifunza Biblia hutuandaa kuelekea mbinguni. Ushindi unakuja kwa kuhubiriwa Injili na kuishika kwa imani.