YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Machi 2021Sample

Soma Biblia Kila Siku Machi 2021

DAY 9 OF 31

Historia ipo ili kutukumbusha yaliyopita. Yataka kutufundisha ili tusirudie mabaya yaliyotangulia. Katika Biblia hakuna linalofichwa. Inatupa mifano hai ya watu na tabia zao ili kutuonya sisi.Mambo hayo waliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani (m.11). Changamoto za sasa za maisha zisiwe chachu mbaya ya kukufanya ukengeuke na kuiacha imani ya Kristo. Jifunze Neno la Mungu ili kumkaribia. Hivyo utapata uimara wa kushinda majaribu yote, maana Mungu ni mwaminifu. Ametupatia mbinu ya kushinda majaribu. Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili(m.13).