Soma Biblia Kila Siku 11/2025Mfano

Ushawishi wa watumishi wa mfalme wa Siria na miungu yake unaendelea. Lengo ni kuwakatisha watu tamaa. Watu waliokata tamaa ni rahisi kushawishika. Lakini hapa kuna jambo la pekee, kwamba mfalme Hezekia amewaandaa watu na taifa ili wamsikilize Mungu tu na wasijibizane na wageni.Watu wakanyamaza kimya; wala hawakumjibu hata neno moja; maana ilikuwa amri ya mfalme, kwamba, Msimjibu neno.Ndipo Eliakimu, mwana wa Hilkia, aliyekuwa msimamizi wa nyumba ya mfalme, na Shebna, mwandishi, na Yoa, mwana wa Asafu mwenye kuandika tarehe, wakaenda kwa Hezekia, na nguo zao zimeraruliwa, wakamwambia Hezekia maneno ya yule amiri(m.21-22). Watu wa Mungu wanajua wanachokiamini kuwa ni cha kweli. Ahadi za Mungu ni za kuaminiwa. Kitu kinachomtofautisha Mungu na miungu ni utendaji na uaminifu wake. Mungu pekee ndiye anayeliokoa taifa, kama anavyosema mwenyewe katika Isa 37:35:Nami nitaulinda mji huu, niuokoe kwa ajili yangu mwenyewe, na kwa ajili ya Daudi, mtumishi wangu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Karibu katika mpango huu wa Soma Biblia Kila Siku mwezi wa Novemba. Utasoma kitabu cha Isaya. Utapata pia maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa na kutafakari Neno ulilosoma. Katika mpango huu, nukuu zote za Biblia zimenukuliwa kutoka katika Swahili Revised Union Version (SRUV).
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz

