Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 07/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 07/2025

SIKU 16 YA 31

Petro, mtume wa Yesu Kristo, kwa wateule wa Utawanyiko, wakaao hali ya ugeni(m.1). Aliowaandikia mtume Petro walikaa sehemu mbalimbali (utawanyiko) katika eneo liitwalo Uturuki siku hizi. Walikuwa katika hali ya ugeni, maana ni wenyeji wa mbinguni. Petro anawaambia kuwa wamepataurithi usioharibika, usio na uchafu, usionyauka, uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu(m.4). Mwampenda[Yesu], ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamwoni sasa, mnamwamini; na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu, katika kuupokea mwisho wa imani yenu, yaani, wokovu wa roho zenu(m.8-9). Walikuwa na sifa gani? Wamezaliwa mara ya pili, wametakaswa na Roho, wamenyunyiziwa damu ya Yesu Kristo, wametii. Petro anawaeleza:Mungu Baba alitangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho, hata mkapata kutii na kununyiziwa damu ya Yesu Kristo. Neema na amani na ziongezwe kwenu. Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu(m.2-3). Hizi ni sifa zako pia? Barua hii ina mambo makuu 3:Tumaini,matesonaushahidiwa Wakristo! (Ukipenda, rudia m.3-5 kuhusu tumaini, na m.6-7 kuhusu mateso).

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2025

Soma Biblia Kila Siku 07/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Julai pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Isaya na 1 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz

Mipangilio yanayo husiana