Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 07/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 07/2025

SIKU 21 YA 31

Hapa tunakumbushwa tena juu ya nafasi nzuri tuliyopewa kama Wakristo kwa rehema zake Mungu. Tumepewa sifa kubwa za ajabu. Tafakari ilivyoandikwa katika m.9-10:Ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema. Lakini ni lazima pia tuelewe kwamba kwa nafasi hiyo tumepewa wito maalumu kwa maisha yetu! Yaani tuwe mashahidi wa Yesu kwa maneno na matendo! Zingatia yafuatayo:mpate kuzitangaza fadhili zake(m.9).Wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu(m.12).Kwa kutenda mema mzibe vinywa vya ujinga vya watu wapumbavu(m.15).Waheshimuni watu wote(m.17).

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2025

Soma Biblia Kila Siku 07/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Julai pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Isaya na 1 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz

Mipangilio yanayo husiana