Soma Biblia Kila Siku 07/2025Mfano

Hapa mtume Petro hufundisha juu yaushahidiwa Wakristo jinsi unavyotakiwa kuonekana katika mwenendo wao. Wametoka tayari katika hali moja (tamaa za kwanza- mwenendo usiofaa) na kuingia katika hali nyingine (watoto wa Mungu - wageni duniani). Kwa hiyo wanapaswa waishi sawasawa na hiyo hali mpya waliyoipata. Wamekuwa watoto wa aliye Mtakatifu kwa hiyo wawe watakatifu kwa mwenendo waowote! Wamekuwa wenyeji wa Mbinguni, kwa hiyo wafikirie na kutumaini sana mambo ya Mbinguni.Vifungeni viuno vya nia zenu, na kuwa na kiasi; mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo(m.13).
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Julai pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Isaya na 1 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz
