Soma Biblia Kila Siku 07/2025Mfano

Tunazidi kufundishwa juu ya mwenendo wetu. Petro anatuagiza tupendanekwa moyo(m.22)! Ila kila wakati hachoki kutukumbusha pia juu ya wokovu wa Mungu katika Kristo. Maana hujua kwamba nguvu ya kuishi maisha mapya hatunayo sisi wenyewe. Nguvu ya Roho twapata tena na tena tunapomfikiria Yesu Kristo jinsi alivyotufia msalabani, na jinsi alivyofufuka. Kwa Kristo mmekuwa wenye kumwamini Mungu, aliyemfufua katika wafu akampa utukufu; hata imani yenu na tumaini lenu liwe kwa Mungu. ... Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele(m.21 na 23. Pia m.2-3, 11 na 18-19 inathibitisha hiyo; tafuta mwenyewe kusoma mistari hiyo)! Lazima tuhubiriwe Kristo na damu yake tena na tena ili tujazwe na Roho wa kweli. Jambo hili linathibitishwa na Paulo, akiandika:Neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu(1 Kor 1:18).Vilevile anapouliza:Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa? Nataka kujifunza neno hili moja kwenu. Je! Mlipokea Roho kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani? Je! Mmekuwa wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho, mnataka kukamilishwa sasa katika mwili?(Gal 3:1-3)
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Julai pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Isaya na 1 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz
