Soma Biblia Kila Siku 07/2025Mfano

Neno la Mungu juu ya maangamizi lilianzia Babeli, likaishia Tiro. Tiro ulikuwa mji wenye bandari maarufu. Umaarufu wake ulitokana na uhusiano wa kibiashara kati yake na nchi nyingi kama vile Misri. Utajiri wa mji ukaongeza uovu uliopindukia. Linganisha na Mungu alivyomwagiza Yeremia kuwakemea:Wafalme wote wa Tiro, na wafalme wote wa Sidoni, na wafalme wote wa kisiwa kilicho ng'ambo ya pili ya bahari ... Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nyweni, na kulewa, na kutapika, na kuanguka msiinuke tena, kwa sababu ya upanga nitakaoupeleka kati yenu(Yer 25:22, 27). Kwa maana siku imewadia kuwaangamiza Wafilisti wote na kuwakatilia mbali walionusurika wote ambao wangeweza kusaidia Tiro na Sidoni. Bwana atakaribia kuwaangamiza Wafilisti, mabaki toka pwani za Kaftori(Yer 47:4 NENO). Nchi za jirani zilitegemea sana Tiro. Uovu na kiburi chake kikasababisha uharibiwe. Watu walimwacha Mungu. Kiburi kinawatenga watu na Mungu. Tujipime, mafanikio yetu yasitutoroshe kutoka kwa Mungu aliye mtakatifu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Julai pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Isaya na 1 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz
 Pata programu
Pata programu
