Soma Biblia Kila Siku 07/2025Mfano

Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu(m.2)."Maziwa yasiyoghoshiwa"ina maana ya maziwa yasiyochanganywa, maziwa safi."Maziwa ya akili", tafsiri nzuri zaidi ni "maziwa ya neno". Mtoto mchanga huhitaji maziwa ili akue vizuri! Ukimpa maziwa yasiyo safi au pombe, mwili wake utadhoofika. Vilevile Mkristo asitamani tena mambo yasiyo safi ambayo amekombolewa nayo. Kwa hiyo Petro anaandika:Wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote(m.1). Badala ya kutamani mambo hayo mabaya, Mkristo alitamanineno, ili kwa hilo akue katika imani!
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Julai pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Isaya na 1 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz
