Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mbazi za YesuMfano

The Parables of Jesus

SIKU 27 YA 36

WAFANYAKAZI WA SHAMBA LA MIZABIBU
Unaposoma mbazi hii, unamuunga mkono nani, wafanyakazi ama mwenye shamba? Unajipata ukifikiri kwamba hawakufaa kupata mshahara sawa ama unamtetea mwenye shamba kwa kulipa alivyolipa?

Mbazi hii ni ya kuonyesha hisia zako kuhusu juhudi zetu na jinsi Mungu alivyotukubali. Waefeso 2:9 inatukumbusha kwamba, "wokovu si tuzo la matendo mema tuliyoyatenda, kwa hivyo hakuna anayeweza kujigamba." Hata hivyo, kuna wengi ambao wanajivunia kazi wanaofanyia Mungu, na kudai walipwe "wanavyostahili" kwa kufanya kazi hiyo "njema!"

Mwenye shamba katika hadithi hii ni mwenye haki; anampa kila mfanyakazi kama alivyowaahidi, na anavyoona inafaa. Vivyo hivyo, Mungu, anatupa neema na rehema kwa sababu ya upendo wake wala si kwa sababu ya juhudi zetu. Lakini, sisi ni aina gani ya wafanyakazi? Tunaona matendo yetu kuwa bora zaidi ya wengine, na kwa hivyo kutarajia kutuzwa zaidi? Tungependa kulalamika tunapowaona wengine wakifanya kidogo ilhali wanapata neema sawa nasi?

Ama tunamshukuru Mungu kwa kutukubali sote? Tunakumbuka kwamba hatumdai Mungu chochote wala lolote, ilhali anatupa kila kitu? Neema na rehema ya Mungu haina mipaka, kwa hivyo tusiwe na wivu ama tuvunjike moyo tunapoona jinsi Mungu anavyowapa wengine. Badala yake, tuzidi kushangilia kwamba Mungu anatuchagua!

Kuhusu Mpango huu

The Parables of Jesus

Mpango huu utakuwezesha kusoma mbazi za Yesu na kuchunguza maana ya mafunzo yake kwako! Unaweza kuendelea na mpango wako ulipoachia kwani imerahisishwa kufika ulipokuwa. Hii itakupa wakati kutafakari na kuhamasishwa na upendo na nguvu wa Yesu!

More

We would like to thank Trinity New Life Church for this plan. For more information, please visit: http://www.trinitynewlife.com/