Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mbazi za YesuMfano

The Parables of Jesus

SIKU 26 YA 36

TAJIRI NA LAZARO
Katika mbazi hii, Yesu anatupa mafunzo mawili: ya kwanza ni kuhusu matumizi ya mali yetu, na ya pili ni iwapo tunaamini Maandiko.

Katika sehemu ya kwanza ya mbazi hii(mistari 19-26) tunaona kwamba hatima ya watu wawili inabadilika wanapofariki. Lazaro ambaye alitamani kupewa makombo yaliyoanguka kutoka mezani anachukuliwa na malaika na kuwekwa karibu na Ibrahamu. Tajiri, ambaye hakushugulika na maskini, anapoaga dunia anapata kwamba atateseka milele. Umuhimu wa mbazi hii si kutufunza kuhusu ahera bali ni kutuonyesha jinsi ni muhimu tutumie mali yetu, ya kiasi yoyote, kupenda na kutunza wenzetu, bali si kupata vitu vyote tunavyotamani. Utajiri, hata ukwasi wa kupindukia, si mbaya bali tunafaa kuwa waangalifu kwa matumizi ya mali hayo. Tunayatumia kujenga Ufalme wa Mungu ama ni kutosheleza tamaa zetu?

Tajiri alipofahamu kosa lake, alitamani kuwaonya ndugu zake ili nao wasiteseke, lakini Ibrahimu anamkumbusha kwamba walishaonywa kupitia Maandiko. Tajiri ana uhakika kwamba miujiza itawawezesha kubadili nia, lakini Ibrahimu hakubaliani naye. Tusijipate katika mtego ambao tajiri alijipata, ya kutafuta ishara ilhali tunapuuza maneno ya Mungu ambayo tunayo mbele yetu. Yesu alifanya matendo mengi ya ajabu alipokuwa duniani, lakini si kila mtu alimwamini na kumfuata. Tunafaa kuwa na shukrani kwamba tumeonywa (hata zaidi ya huyo tajiri) katika Maandiko bila kudai kwamba Muumba atupe zaidi.

Kuhusu Mpango huu

The Parables of Jesus

Mpango huu utakuwezesha kusoma mbazi za Yesu na kuchunguza maana ya mafunzo yake kwako! Unaweza kuendelea na mpango wako ulipoachia kwani imerahisishwa kufika ulipokuwa. Hii itakupa wakati kutafakari na kuhamasishwa na upendo na nguvu wa Yesu!

More

We would like to thank Trinity New Life Church for this plan. For more information, please visit: http://www.trinitynewlife.com/