Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mbazi za YesuMfano

The Parables of Jesus

SIKU 28 YA 36

WANA WAWILI, MMOJA PEKEE ATII
Mbazi hii ambayo ni fupi na dhahiri inatupa changamoto ya kuhakikisha kwamba maneno yetu na nia zetu zinaambatana na matendo yetu. Mara nyingi katika maisha yetu kama Wakristo, maneno yetu ni mazuri mbele ya watu lakini matendo yetu ya kibinafsi hayaafikiani na maneno yetu.

Maisha ya Mkristo si maneno yetu pekee, wala katika fikra zetu pekee, au moyoni mwetu pekee, ama katika matendo yangu pekee. Maisha ya Mkristo ni vitu hivyo vyote pamoja ili kufunzwa, kutii, na kufunza wengine kuhusu Yesu.

Ikiwa nia zako za kindani na matendo yako yanaoonekana haziambatani, usihalalishe tabia yako kwa kusema, "hakuna aliye kamili," "mimi si kamili bali aliyesamehewa," ama kisingizio kikuu, "ni Mungu pekee anayeweza kunihuku!" Badala yake, tubu kiburi chako, omba Mungu akupe neema na rehema ili ugeuzwe, na uruhusu ufunzwe ili umtukuze Mungu kindani na nje.

Kuhusu Mpango huu

The Parables of Jesus

Mpango huu utakuwezesha kusoma mbazi za Yesu na kuchunguza maana ya mafunzo yake kwako! Unaweza kuendelea na mpango wako ulipoachia kwani imerahisishwa kufika ulipokuwa. Hii itakupa wakati kutafakari na kuhamasishwa na upendo na nguvu wa Yesu!

More

We would like to thank Trinity New Life Church for this plan. For more information, please visit: http://www.trinitynewlife.com/