Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 02/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 02/2025

SIKU 3 YA 28

Mungu si kama sisi. Habadiliki, rehema yake inaendelea, naye ni mwaminifu kabisa. Tena ni mtawala wa vitu vyote, yaani hakuna awezaye kumwangusha Mungu wala rehema yake. Bwana peke yake anastahili kuhimidiwa, lakini ni kana kwamba sauti ya mtunga zaburi haitoshi, kwa hiyo anawakaribisha malaika washiriki, na pia matendo yote (viumbe vyote) ya Bwana. Hivyoitakayosikika ni sifa tu kwa Bwana. Daudi anaona amezidiwa na fadhili na rehema za Bwana, hajui la kusema. Kwa hiyo anasema:Vyote vilivyo ndani yangu vilihimidi jina lake takatifu!(m.1) Wewe unasemaje?

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 02/2025

Soma Biblia Kila Siku 02/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Zaburi na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz