Soma Biblia Kila Siku 02/2025Mfano

Daudi anaendelea kutaja fadhili za Bwana kwa watu wake. Mwanzo wa matendo yote ni haki ya Mungu na kwambaBwanaamejaahuruma na neema(m.8). Ndivyo anavyojifunua kwako. Na Daudi anashuhudia kwamba kiini cha fadhili za Mungu ni kwamba anapenda kutupa ondoleo la dhambi.Hakututenda sawasawa na hatia zetu, wala hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu(m.10). Katika m.11-12 Daudi anataja urefu wa aina mbili: kati ya mbingu na nchi (mbingu zilivyoinuka juu ya nchi), na kati ya mashariki na magharibi (mashariki ilivyo mbali na magharibi). Nani anaweza kupima marefu haya? Hakuna!Ndivyo Mungu alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.Kumbuka daima kwambarehema ya Mungu kwako haina vipimo. Mungu anafahamu udhaifu wetu, bila rehema yake hatuwezi kudumu.Kwa maana Yeye anatujua umbo letu, na kukumbuka ya kuwa sisi tu mavumbi(m.13-16).
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 02/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Zaburi na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz